Image
Image

Mifuko 5,319 ya Shehena ya Sukari ya Magendo imetaifishwa na (TRA) Mkoani Lindi.

Mamlaka ya Mapato (TRA) Lindi imetaifisha na kugawa sukari mifuko 5,319 toka Brazil yenye thamani ya Sh 373.5 milioni na kuigawa kwa taasisi mbalimbali mkoani humo ikiwa ni sehemu ya shehena iliyokamatwa ikiingizwa kimagendo nchini mwezi Februari 2016.
Sukari hiyo ilikamatwa mwezi wa pili mwaka huu katika bandari ya Lindi ikiingizwa nchini kinyume cha sheria kutoka Brazil kupitia bandari ya zanzibar.
Akizungumza wakati wa
ugawaji wa sukari hiyo kwa taasisi za serikali mkoa wa Lindi Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi TRA- Richard Kayombo amesema wamelazimika kuchukua hatua kulingana na sheria inavyowataka.
Amesema makubaliano hayo yalifikiwa baina ya TRA na serikali ya mkoa baada ya wenye mali kushindwa kulipa faina na kukomboa mzigo huo ambao mbali na sukari pia meli hiyo ilibeba mafuta ya kupikia,baiskeli,biskuti amira na bidhaa nyingine.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Lindi Hayaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi amesema serikali ya mkoa huo imejipanga vizuri kiulinzi na kuwaasa wafanyabiashara wa mkoa huo kufanya biashara kwa kufuata sheria za nchi vyinginevyo wataishia pabaya.
Taasisi zilizopata sukari hiyo ni magereza, shule maalumu, kambi ya wazee, shule za kawaida,hospitali na magereza.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment