Chama cha Alliance for Democratic Change ADC kimewafuta uwanachama wanachama wake wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama
hicho Bwana Said Miraaj,Katibu Mkuu Bi.Lydia Bendera,Mkurugenzi wa
mipango na uchaguzi Bwana Jumanne Magafu pamoja na Katibu wa Kamati ya
ulinzi Bwana Juma Wandwi kwa makosa ya kukiuka katiba ya chama hicho kwa
kususia kushiriki uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar.
Maamuzi hayo yamefikiwa katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo akizungumza baada ya ufunguzi aliyekuwa mlezi
wa chama cha ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Zanzibar,Mhe.Hamad
Rashid amesema katiba ya chama inasisitiza ushiriki katika kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi,hivyo kutoshiriki ni kukivunja nguvu chama
katika mikakati yake ya kuchukua dola.
Akizungumza na wajumbe wa
mkutano mkuu wa -ADC- Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa Bwana Sisty
Nyahoza amesema kitendo cha chama cha siasa kutoshiriki uchaguzi
kinakwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa na malengo ya kuanzishwa chama Chopchite cha siasa na kusisitiza hipo haja ya kuangalia mfumo wa usajili wa vyama utakaowezesha kutoa adhabu kwa vikavyoonekana kukataa kushiriki katika chaguzi.
Aidha mkutano mkuu huo wajumbe wamemchangua aliyekuwa mlezi wa ADC ambaye kwa sasa ni Waziri wa Kilimo Zanzibar Mhe.Hamad Rashid kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Doyo Hassan Doyo amechaguliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu wa chama.
Home
News
Slider
Wanachama 4 akiwamo Mwenyekiti wa ADC wafutwa uanachama kususia uchaguzi wa marudio Zanzibar.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment