Zaidi ya tani 154 za sukari inayodaiwa kufichwa kwenye Maghala na mfanyabiashara mkubwa wa bidhaa hiyo mkoani Dodoma zimezuiliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)
na maofisa wa jeshi la Polisi ili kupisha uchunguzi na endapo
itabainika kuwa ilifichwa makusudi muhusika atachukulia hatua kulingana
na maagizo yaliyotolewa na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.John Pombe Magufuli.
Shehena hiyo inabainika kufuatia msako uliofanywa usiku na TAKUKURU na Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa ya uwepo
wa sukari kwenye maghala hayo ambapo mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma
Emma Kuhanga amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na endapo
itabainika kuna hujuma ndani yake hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi
ya muhusika.
Kwa upande wake mmoja kati ya watunza ghala aliyefahamika kwa jina maoja la samir aliyekutwa eneo la tukio wakati wa msako huo amekanusha kuwa sukari hiyo imefichwa huku akidai kuwa inauzwa sokoni kila siku kwa utaratibu maalum.
Wakati
sakata la uhaba wa sukari likiendelea kutikisa nchi nzima jukwaa huru
la wazalendo tanzania limetoa tamkoa la kulaani wafanyabiashara
wanaohujumu upatikanaji wa bidhaa hiyo huku makundi mbalimbali ya jamii
yakiendelea kupaza sauti kuitaka serikali itafute suluhisho mapema kwani wanaoumia asilimia kubwa ni wananchi wa maisha ya kawaifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment