Wadau wa Mto Ruaha Mkuu, wameafikiana kupanga mpango wa pamoja utakatekelezwa kwa pamoja ili kurejesha mtiririko wa maji katika mto huo kwa mwaka mzima.
Mto Ruaha Mkuu ndiyo chanzo cha maji ya bwawa la mtera ambalo huzalisha megawati 80 na bwawa la Kidatu ambalo huzalisha megawati 204 za umeme wa gridi ya Taifa.
Mto Ruaha Mkuu ndiyo chanzo kikuu cha maji kwa watu na wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pia unashikilia maisha ya zaidi ya watu milioni moja kupitia kilimo cha umwagiliaji na uvuvi katika eneo bonde la Mto huo.
Katika Kikao cha wadau kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira na mali hai Duniani la WWF,kwa mara nyingine wadau hao wanakiri kuwa ni hatari kubwa kwa Mto huo kuachwa uendelee kukauka
Kaimu Meneja wa kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera,Mhandisi Lewis Loiloi amesema ikiwa Mto Ruaha utakauka kabisa basi gridi ya Taifa itaondokewa na Megawati za umeme 284 huku Mkuu wa Mkoa wa Iringa akionya kuwa migogoro michache ya kugombea maji inayoendelea katika baadhi ya maeneo inaweza kuwa mikubwa na kugeuka ya wilaya na wilaya kama hali ya kukauka kwa mto Ruaha Mkuu kutaendelea
Mkutano huo uliohudhuriwa na Mikoa minne ya Iringa,Njombe, Mbeya na Dodoma na viongozi wa Wizara zinazoshughulika na Maji,Ardhi na Mazingira, utafanyika tena kati ya mwezi wa nane na wa tisa kufanya tathmini ya mambo waliyokubaliana ikiwa suala la Mpango huo wa pamoja.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment