Image
Image

Iran kuzamisha meli za kivita za Marekani iwapo zitakuwa tishio kwa nchi hiyo.

Kamanda katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran IRGC ameonya kuwa jeshi hilo linaweza kuzamisha meli za kivita za Marekani iwapo zitakuwa tishio kwa nchi hii.
Kamanda wa Kikosi cha Majini cha IRGC Admeri Ali Fadavi amesema kila wakati Wamarekani wanapoangalia Ghuba ya Uajemi wanaona vikosi vya Iran na akaongeza kuwa, "Wamarekani wanafahamu kuwa, iwapo watafanya hata kosa dogo kabisa, tutazamisha meli zao za kivita Ghuba ya Uajemi, Lango la Hormoz na Bahari ya Oman."
Kamanda huyo ameashiria uwezo mkubwa wa Jeshi la Wanamaji la Iran na kusema maadui wa Iran wanafahamu tu sehemu ndogo ya uwezo wa kijeshi wa Iran.
Admeri Fadavi ameongeza kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lina maghala ya chini ya ardhi yenye makombora ya nchi kavu kwa bahari. Aidha amesema kuna boti nyingi za kivita katika maghala hayo ya chini ya ardhi na hivyo zinaweza kuingia vitani mara moja pasina kukabiliwa na tishio la kulengwa na adui.
Admeri Fadavi amesema hivi sasa kuna karibu meli 60 za kivita za Marekani, Uingereza na Ufaransa katika Ghuba ya Uajemi na kuongeza kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu linafuatilia kila nyendo za manoari hizo za kigeni.
Admeri Fadavi pia amekosoa muswada wa hivi karibuni wa Bunge la Marekani la Kongresi kupinga mazoezi ya kijeshi ya Iran katika Ghuba ya Uajemi. Kamanda huyo mwandamizi wa Iran amesema Marekani au madola mengine hayana uwezo wa kuzuia Iran kufanya mazoezi ya kijeshi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment