Katika toleo lake la leo Jumatano, gazeti la Daily News limeandika makala hiyo chini ya kichwa cha maneno: Wapalestina: Ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ni za mababu zetu.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mapema mwezi uliopita, watu walialikwa katika makazi ya Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem Sabat jijini Dar es Salaam na katika mwaliko huo, hadhirina walioneshwa video ya mateso wanayopata Wapalestina kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Katika sehemu moja ya makala hiyo, mwandishi Lawi Joel ameandika: Picha za ukatili wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na kuharibiwa mali za watu hao wanaodhulumiwa, zilikuwa za kuogofya. Tanzania imekuwa ikilaani vitendo vya kikatili vinavyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina kama ambavyo pia inalaani uvamizi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza.
Aidha mwandishi ameandika: Katika miaka ya 1970 na 80, Tanzania na Wapalestina waliunda tume ya pamoja inayojulikana kwa jina la TPSC kwa ajili ya kuendeleza juhudi za mataifa hayo mawili za kuunga mkono jitihada za kupambana na uhalifu wa kimataifa unaotendwa dhidi ya Wapalestina.
Ijapokuwa nchi nyingi duniani zinaunga mkono haki ya Wapalestina ya kuwa na taifa lao huru, na licha ya Umoja wa Mataifa kusema wazi kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unapaswa kuwarejeshea Wapalestina ardhi zao, lakini hadi leo hii utawala huo ghasibu unaendelea kuonesha jeuri kutokana na uungaji mkono wa madola ya kibeberu hususan Marekani.
0 comments:
Post a Comment