Image
Image

Jeshi la Nigeria lathibitisha kuuawa kwa mtaalamu wa utengezaji mabomu wa Boko Haram.

Jeshi la Nigeria limetoa maelezo na kuthibitisha kuuawa kwa mtaalamu wa utengezaji mabomu wa kundi la Boko Haram.
Msemaji wa jeshi la Nigeria kanali Sani Usman aliarifu kwamba mtaalamu huyo aliuawa kwa kufyatuliwa risasi na wenziwe kwenye kambi ya msitu wa Sambisa.
Mtaalamu huyo anasemekana kwamba alikuwa mmoja wa makamanda wakubwa wanaongoza kundi la Boko Haram.
Mtaalamu huyo alichaguliwa kuwa mhusika mkuu wa utengezaji mabomu na vilipuzi vya Boko Haram baada ya mtaalamu wa zamani aliyetambulika kwa jina la Abu RPG kuuawa miaka ya nyuma.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment