Kenya imetoa sera mpya ya mazingira na usafi inayolenga kusaidia nchi hiyo kuokoa dola za kimarekani milioni 270 kila mwaka kutokana na hali mbaya ya usafi.
Waziri wa afya wa Kenya Bw Cleopa Mailu amesema serikali na wenzi wake wa maendeleo wameanza kupokea mikakati inayosaidiana ili kuwahakikishia wakenya wote wanakuwa na mazingira safi zaidi na afya, na maisha ya hali ya juu yenye heshima.
Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Kenya, ni asilimia 32 tu ya Wakenya waishio vijijini wamepata hali iliyoboreshwa ya usafi, na mmoja kati ya wakenya saba hamna choo.
0 comments:
Post a Comment