Serikali ya Burundi imesema itashiriki kwenye mazungumzo ya amani yenye lengo la kutafuta amani ya Burundi yatakayofunguliwa Jumamosi wiki hii mjini Arusha Tanzania.
Ofisa habari wa Ikulu ya Burundi Bw Willy Nyamitwe amesema mazungumzo hayo ya siku nne yatakayoendeshwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Bw Benjamin Mkapa, yatakuwa na majadiliano na sio kutafuta makubaliano. Amethibitisha kuwa wajumbe kutoka vyama vya siasa na jumuiya za kiraia wamealikwa kwenye mazungumzo, lakini amesisitiza kuwa serikali ya Burundi haitakaa meza moja wajumbe kutoka makundi yanayotumia mabavu.
Hapo awali serikali ya Burundi ilikataa kushiriki kwenye mazungumzo hayo, kwa madai kuwa haikuarifiwa na kuwa haikuwa tayari kuzungumza na makundi yanayotumia mabavu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment