Shirika la Kazi Duniani ILO limesema, ukosefu wa ajira zenye ubora umepunguza matokeo mazuri ya miaka kumi iliyopita katika kupunguza umaskini duniani, pia ni tishio katika kuhimiza mchakato wa maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa.
Ripoti ya mustakabali wa ajira na jamii kwa mwaka 2016 iliyotoewa jana na Shirika hilo imesema, nchi nyingi zinazoendelea zimepiga hatua kubwa katika kupunguza umaskini, lakini kwa kasi tofauti. Ripoti hiyo imesema, nchi za Afrika na baadhi ya nchi za Asia bado zinakabiliwa na umasikini, na kwamba idadi ya watu maskini imeongeza katika nchi zilizoendelea hasa za Ulaya.
Ripoti hiyo imesisitiza kwamba mashirika yanatakiwa kuongeza uwezo wao wa maendeleo endelevu, na kutoa nafasi nyingi za ajira zenye ubora, ili kuondoa umaskini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment