Aliyekuwa
Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa
mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji
la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare April 27 2016 walikosa dhamana
kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa mahakama kuu kupinga maamuzi
ya kupewa dhamana.April
29 2016 kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es salaam ambapo awali Hakimu Mchauru alitoa maamuzi ya
kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka Mei 12 mwaka huu, sababu ni kutokana na
jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kukatwa kwa rufaa
ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.
Muda mfupi
baadae majira ya saa 4;30 asubuhi walirudishwa tena mbele ya Hakimu
Mchauru baada ya kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es salaam akitamka kesi hiyo itajwe Mei 3 mwaka huu badala ya
mei 12, aliyoipanga awali.
Sasa Leo 3 May 2016 ambapo Mahakama ya
Hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ilipanga kusikiliza kesi hiyo kutokana
na jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu kurudi leo lakini
halijarudi hivyo kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 18 2016 watuhumiwa
wamerudishwa rumande.
Hata hivyo watuhumiwa walitakiwa kufika
mahakama Kuu kwa ajili ya kuendelea na rufani ambapo baada ya kufika
Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kuanza kusikiliza rufani
hiyo May 5 2016.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment