Wakati
sekeseke la kutooneshwa mijadala inayoendelea Bungeni kupitia
Television(Runinga) ya Taifa TBC LIVE bado linaendelea kuchukua Sura
mpya kila uchao ambambo aliyekuwa Waziri mkuu mstaafu nchini Tanzania
Frederick Sumaye naye amelaani kitendo hicho nakusema ni ukiukwaji wa
haki ya msingi ya kikatiba za kutoonesha Bunge nakuwanyima watanzania
haki ya msingi ya kufuatilia mijadala inayoendelea Bungeni.
Mh.Sumaye
ameyasema hayo Leo ikiwa nikilele cha Uhuru wa vyombo vya habari
duniani ambapo pamoja na mambo mengingine ameonekana kuguswa na kitendo
cha matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni kutorushwa kwani wakati
yalipokuwa yakirushwa yalikuwa yakiwasaidia wananchi kufahamu na
kuyaelewa mambo muhimu yanayohusu nchi, kupata taarifa za maeneo mengine
zinazowasilishwa na wabunge na kuona namna ambavyo wawakilishi wao
wanavyowawakilisha wakiwa Bungeni mjini Dodoma kwa walicho watuma.
Hata
hivyo Sumaye amesema "hatua hiyo inavunja katiba na kuminya baadhi ya
taarifa zisiwafikie wananchi na kutoa taarifa ambazo tu utawala
umeridhia"Alisema Sumaye.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kiujumla
hali ya vyombo vya habari duniani bado inakutia shaka ambapo takribani
wana habari 800 wameuawa duniani ikiwa ni kwa kipindi cha tangu mwaka
2012 mpaka leo, huku wengine wakitekwa au kupotea.
Siku ya uhuru wa
vyombo vya habari duniani ilitangazwa na baraza la umoja wa mataifa
mwaka 1993, kwa lengo la kutathimini uhuru wa vyombo vya habari ukoje,
kuvilinda vyombo vya habari dhidi ya mashambulizi ya wale wasiotaka
maovu yao kufichuliwa na kukumbuka waandishi wa habari waliopoteza
maisha yao wakiwa katika kazi zao.
Home
News
Slider
SUMAYE:Kutokuoneshwa Bunge ni ukiukwaji wa Katiba na kunaminya uhuru wa habari na wananchi kupata habari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment