WAKATI
tukikumbuka kifo cha mfalme wa muziki wa reggae, Robert Nesta ‘Bob
Marley’, aliyefariki Mei 11, 1981 huko Miami kumbukumbu haifutiki inapo
nijia sura yake, muziki wa reggae kwa Tanzania unaonekana kushuka kutokana na sababu mbalimbali.
Wanamuziki
waliokuwa wakiimba muziki huo wengi wao wanaendeleza harakati nyingine
tofauti na walivyokuwa wakifanya zamani kwa kuuendeleza muziki huo kwa
kutoa nyimbo mbalimbali zenye mafunzo, hamasa na umoja.
Lakini wapo
wengine wanauendeleza muziki huo kwa kuendelea na kutoa nyimbo
mbalimbali lakini wanakosa nafasi ya kuchezwa kwenye vituo mbalimbali
vya redio nchini kutokana na sababu pia mbalimbali ikiwemo kutokuwa na
vipindi vya kutosha vya kucheza muziki huo, pia kutokuwa na weledi wa
waandaaji wa vipindi hivyo au kukosa hamasa kwa wasikilizaji wa vituo
vya redio na runinga.
Kitu kikubwa kilichotakiwa na wanamuziki hao wa
reggae ni kutokata tamaa kwa muziki wao kwa kuwa hata waanzilishi
walianza muda mrefu bila mafanikio lakini baadaye walipata mafanikio
makubwa kiasi kwamba kwa leo tunakumbuka kumbukumbu zao licha ya
kufariki dunia.
Bob Marley alizaliwa Februari 6 mwaka 1945 huko Nine Mile, Saint Ann Parish nchini Jamaika.
Inaelezwa
kwamba jina lake halisi ni Nesta Robert Marley, lakini kutokana na
kukosewa kwa majina yake katika hati ya kusafiria akaendelea kutumia
jina la Robert Nesta Marley.
Mama yake alikuwa mweusi, alifahamika
kwa jina la Cedella Booker na baba alikuwa Mzungu aliyefahamika kwa jina
la Norvall Marley, lakini baba yake alifariki mwaka 1955 kwa ugonjwa wa
moyo akiwa na miaka 10 tu baada ya kifo hicho akawa akilelewa na mama
yake.
Mama yake anaolewa tena
Licha
ya kupenda muziki lakini alipokuwa na umri wa miaka 12, mama yake
alimchukua Bob Marley wakahamia katika Jiji la Kingston ambako
alianzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine, akapata watoto
wawili, Bunny Wailer na binti yake Pearl.
Bob na Bunny wakaungana na
kuendeleza muziki kwa kuiga muziki waliokuwa wakiusikiliza redioni,
baadaye walikutana na Peter Tosh, Beverley Kelso na Junior Braithwaite
na baadaye wakawa maarufu wakubwa duniani.
Februari 1962 nyimbo wa
‘Judge Not’, ‘One Cup of Coffee’, ‘Do You Still Love Me?’ na ‘Terror’
zilitungwa na kuingizwa sokoni na mwaka mmoja baadaye, Bob Marley, Bunny
Wailer, Peter Tosh, Junior Braithwaite, Beverley Kelso na Cherry Smith
wakaanzisha kundi la The Teenagers ambalo walilibadilisha na kuliita The
Wailing Rudeboys kisha The Wailers.
Mwanzoni mwa mwaka 1964 waliuza
nakala 70,000 wakati huo. The Wailers likawa kundi kubwa lakini mwaka
1966 baadhi ya wanamuziki walilikacha kundi hilo na kuwaacha wakongwe
Bob Marley, Bunny Wailer na Peter Tosh.
Alijifunzaje muziki
Wakiwa
shule ya msingi ya Stepney iliyopo Nine Mile, alikutana na rafiki yake
Neville Livingston maarufu kwa jina la Bunny Wailer, kidogo kidogo
walianza kujifunza muziki hadi walipoingia sekondari.
Ndoa na imani
Mwaka 1966, Bob Marley alimuoa Rita Anderson ambaye alijiunga katika kundi lake akiwa kama mwimbaji mwitikiaji.
Baadaye
walihamia kwa muda nchini Marekani katika Jiji la Delaware huko akawa
mfanyakazi katika kiwanda cha kutengenza magari cha Chrysler akawa
akijiita Donald Marley huku akiendeleza imani ya kirastafari.
Aliporudi
Jamaica akaingia rasmi katika Urastafarian na kuanza kufuga nywele kwa
mtindo wa ‘dreadrocks’ imani hii ya kufuga nywele bila kukata inadaiwa
inatokana na maelezo ya Biblia kuhusu Samson aliyeelezwa kwamba alikuwa
na guvu za siri katika nywele zake za asili.
Mwaka 1976, Marley
aliondoka Jamaica, akahamia Uingereza kati ya mwaka 1977 mpaka 1978
akiwa huko alirekodi albamu mbili ya Exodus na Kaya. Exodus ilikuwa
kwenye chati za Uingereza kwa wiki 56 yaani mauzo yake yalikuwa kati ya
albamu bora kwa wiki 56. Inasemekana aliuza nakala milioni 75 za albamu
hiyo.
Siasa
Mwaka
1978 alirudi tena Jamaica kufanya concert jingine la amani lililoitwa
‘One Love Peace Concert’, mwisho wa onyesho kwa maombi ya Bob, viongozi
wa kisiasa waliokuwa wakipingana na kupelekea wafuasi wao kuuana,
Michael Manley (kiongozi wa chama kilichokuwa kikitawala wakati huo,
People’s National Party) na Edward Seaga (kiongozi wa upinzani wa chama
cha Jamaica Labour Party), wakashikana mikono.
Bob alirekodi kwa jina
la Bob Marley and the Wailers albamu 11, albamu nne za live na saba za
studio, ikiwemo Babylon by Bus, pia alisaidia maeneo mbalimbali
yaliyokuwa na migogoro ya kisiasa kumaliza migongano yao.
Kifo chake
Julai
1977, Marley akakutwa na kitu kimeota chini ya ukucha wa mguu wake,
kitu kilichoonekana na madaktari kuwa ni aina ya kansa, hivyo daktari
wake akamshauri akatwe kidole lakini alikataa kwa madai kwamba dini yake
hairuhusu.
Mei mwaka 1980, alikuwa ameshakamilisha ziara ya nje ya
nchi lakini alipofika Milan, Italia alifanya onyesho lililohudhuriwa na
watu 100,000, alipomaliza akahamia Marekani akafanya maonyesho kadhaa
lakini afya yake ilianza kuzorota kutokana na kansa kuenea mwili mzima.
Mei
11, 1981, alifariki katika Hospitali ya Cedars Lebanon alipokuwa na
umri wa miaka 36 tu Mei 21 mwaka huo alizikwa na gitaa lake jirani na
alipozaliwa kwa mazishi ya kitaifa na kadiri ya imani yake ya
Urastafarian.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment