Klabu ya Everton imempiga kalamu mkufunzi wake Roberto Martinez baada ya kuifunza klabu hiyo kwa miaka mitatu.
Kilabu
hiyo ya Martinez ilio katika nafasi ya 12 katika jedwali li ligi ya
Uingereza ilishindwa 3-1 na mabingwa wa ligi Leicester siku ya Jumamosi
na kupoteza 3-0 dhidi ya Sunderland siku ya Jumatano.
Everton ilipoteza katika nusu fainali ya kombe la FA na lile la Carling msimu huu.
Timu
hiyo imeshinda mechi tano pekee nyumbani msimu wote na inatarajiwa
kumaliza msimu huu ikiwa na pointi za chini zaidi tangu uzinduzi wa
pointi tatu kwa ushindi wowote mnamo mwaka 1981.
Klabu hiyo
inatarajiwa kuthibitisha rasmi hatua yao.Kumekuwa na ongezeko la
maandamano dhidi ya kocha huyo raia wa Uhispania kutoka kwa mashabiki
katika mechi zilizochezwa nyumbani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment