Rais
wa Uganda Yoweri Museveni ameapishwa siku ya Alhamisi kuongoza mhula
mwingine wa miaka mitano, huku kiongozi wa mkuu wa upinzani Kiiza
Besigye akikamatwa na mitandao ya kijamii kuzimwa.
Rais Museveni
mwenye umri wa miaka 71, ambaye ameitalwa Uganda tangu 1986, alichukuwa
asilimia 60 ya kura katika uchaguzi mkuu uliyofanyika mwezi Februari. "
Waganda wamekuwa wakishiriki uchaguzi wa vyama vingi kwa miaka kadhaa
sasa na katika uchaguzi wa mwisho alieshinda ni mgombea Museveni na
ndiyo maana anaapishwa hii leo," alisema Badru kiggundu, mwenyekiti wa
tume ya taifa ya uchaguzi nchini Uganda.
Chama kikuu cha upinzani cha
Forum for Democratic Change FDC, ambacho kinasema matokeo ya uchaguzi
huo yalichakachuliwa, siku ya Jumatano kilifanya hafla yake ya siri ya
kumuapishwa mgombea wake Kizza Besigye, ambayo ilisambaa kwenye mtandao
wa Youtube.
Besigye amkuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu
ulipomalizika uchaguzi huo, kulingana na msemaji wa aFDC Ibrahim Semuju
Nganda. Polisi inasema uzuwiaji huo unalenga kuhakikisha besigye hatendi
makosa. Baada ya vidio ya kuapishwa kwake kutolewa, Besigye aliwapiga
chenga walinzi wake na kuingia mitaani, hatua iliyolilaazimu jeshi la
polisi kumkamata.
Besigye kushtakiwa kwa kukaidi "amri halali"
"Alikuwa
anaongoza kundi la watu kuvuruga amani," alisema Patirick Onyango,
msemaji wa jeshi la polisi na kuongeza kuwa, "tutamshitaki kwa kukaidi
amri halali." Wanachama wengine wa upinzani pia walikamatwa kuelekea
kuapishwa kwa Museveni, kwa mujibu wa duru kutoka upande wa upanzani.
Siku
ya Jumatano serikali iliizima mitandao ya kijamii ya Facebook, twitter
na WhatsApp, ambapo watumiaji walishindwa kuingia kwenye akaunti zao za
mitandao hiyo. Msemaji wa mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano ya Uganda,
UCC alikamataa kuzungumzia hatua hiyo.
Polisi wa kuzuwia fujo
walisambazwa katika maeneo mengi ya mji wa Kampala ambako maduka mengi
yalisalia kufungwa, baada ya hapo Jumatano kuwatembezea kichapo wakaazi
waliompungia mikono Kizza Besigye.
Miongoni mwa viongozi wa Kiafrika
waliohudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Museveni ni pamoja na rais wa
Sudan Omar Hassan al-Bashir, anaetafutwa na mahakama ya kimataifa ya
uhalifu ICC kwa makosa ya uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.
Museveni amepuuza wito wa kukamatwa kwa al-Bashir, akiitaja ICC kuwa
kundi la watu wasio na maana.
Ingawa viongozi wa Afrika awali
walikaribisha hatua ya kuanzishwa kwa mahakama ya ICC, walikuja kuigeuka
pale ilipoanza kujaribu kuwawajibisha. Wakati Museveni akiitaja ICC
kuwa kundi la watu wasio na maana, rais al-Bashir alikuwa akitikisa
kichwa katika ishara ya kukubaliana naye.
Aishukuru Urusi kwa mauzo ya silaha bila masharti
Museveni
pia aliishukuru Urusi kwa utayarifu wake kuiuzia Uganda silaha, "bila
masharti na jeuri kama mataifa mengine," na kuahidi kuanzisha vita dhidi
ya rushwa. " Ukiniona nimevaa tai unasahau kuwa niliwahi kuwa muasi?"
aliuliza.
Viongozi wa mataifa ya Chad, Ethiopia, Afrika Kusini, Sudan
Kusini, Tanzania na Zimbabwe pia walihudhuria sherehe hiyo. Baada ya
kuapishwa kwake, Museveni aliendelea kusimama kwenye jukwaa nyumba ya
bilauri zisizopitisha risasi, na kukabishiwa zana kadhaa za mamlaka,
zikiwemo mhuri wa rais na benedera ya taifa.
Baadae bendi za jeshi
zilitumbuiza, na mizinga 21 ilifyatuliwa, wanajeshi wakafanya gwaride na
ndege za kivita zilifanya maonesho angani huku makundi ya waliohudhuria
yakitazama.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment