Image
Image

UTAFITI:Asilimia 80 ya watoto wanakabiliwa na tatizo sumu kwenye damu nchini Tanzania.

Tafiti za kitaalam zimeonyesha zaidi ya asilimia 80 ya watoto nchini wanakabiliwa na tatizo la kuwa na sumu kwenye damu kufuatia ulaji wa vyakula vyenye vimelea vya fangasi huku mazao ya karanga, maziwa na mahindi yakitajwa kuongoza kwa kuwa na vimelea hivyo vya fangasi za mimea.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasilisha mada ya namna Tanzania inavyoathirika na vimelea hivyo vya fangasi na mipango inayoichukua kama nchi kupambana na hali hiyo mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandele ameyataja maeneo ya Kibaigwa Morogoro na Kilosa, kama moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi na fangasi hizo kwenye mazao. 
Mtafiti huyo amesema licha ya umoja wa Afrika kuanza kuunga mkono juhudi za Tanzania za kupambana na tatizo hilo kwenye mimea, juhudi za makusudi hazinabudi kuchukuliwa kwani jamii itaendelea kuathirika zaidi, na kwamba hata mamlaka za TFDA na TBS haziwezi kudhibiti vyakula vyote vinavyotoka mashambani huku vikiwa vimekwisha kuathirika na vimelea hivyo.  
Kwa upande wa serikali inasema imekwisha kutambua tatizo hilo na kwamba juhudi nyingi zinafanywa za utoaji wa elimu kwa wananchi ya namna ya kukausha mazao yao pindi wanapovuna huku pia ikiahidi kutumia vema ufadhili wa umoja wa Afrika katika kuhakikisha inatokomeza vimelea hivyo kwenye mazao. 
Katika hatua nyingine utafiti uliofanywa na vyuo vikuu vitatu vikiwemo vya Sokoine,  chuo Kikuu cha Dar es salaam, na Chuo Kikuu cha Nkwame Nkuruma cha inchini ghana umebaini kuwa uchanganyaji wa banda la kuku, bwawa la samaki na kilimo cha mbogamboga katika eneo moja kunaweza kusaidia kuondoa umasikini kwa wananchi wa kipato cha chini hasa waishio katika nchi zinazoendelea.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment