Miili ya watu saba wa familia moja waliouawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia 11 May 2016 wanatarajiwa kuzikwa hivi leo kwa gharama za Halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Msemaji wa familia Bw.Simon Mbata na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amesema kuwa maziko yatafanyika mwendo wa kwenye kijiji cha Sima kuliko tokea mauaji sanane mchana leo 13 May 2016.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Zainabu Terack amesema kuwa upelelezi wa tukio unaendelea hivyo nimapema mno kulizungumzia suala hilo ambalo polisi wanaendelea nalo.
"Ninachoweza kuahidi ni kwamba kamati ya ulinzi na Usalama haitapumzika,hadi wauaji wote watiwe mbaroni"alisema Terack.
Kwenye tukio hilo waliouawa ni Mama wa Familia Eugenia Kwitega na watoto wake watatu,Leonard Thomas aliyekuwa akisoma kidato cha nne kwenye shule ya sekondari Sima,Leonard Aloyce na Mkiwa Phillip,wote walikuwa wakisoma shule ya ya Msingi Ijinga.
Wengine ni Maria Phillip ambaye ni mdogo wa mama wa familia hiyo aliyekuwa kafika kijijini hapo kumtembelea dada yake pamoja na wageni wengine wawili waliotambulika kwa jina moja tu la Samson na Donald.
Aidha Polisi imewaomba watu wenye taarifa na watu hao waliofanya tukio la ukatili kushirikiana nao katika kutoa taarifa ili kusaidia kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
TAHADHARI:Picha za watu waliokatwa mapanga zipo humu zinatisha kuziona BOFYAHAPA.->http://bit.ly/1rJiZBc
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment