Leo May 13 2016 aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia sakata la sukari.
Prof. Lipumba amemshauri Rais Magufuli kuruhusu uingizaji wa sukari kutoka nje kwasababu viwanda vyetu vya ndani vya sukari havitoshelezi mahitaji ya sukari kwa wananchi na pia amesema vimesimama kuzalisha sukari kwa zaidi miezi sasa.
Prof. Lipumba amesema ’TAKUKURU badala ya kuwakamata Tegeta Escrow Account wanashughulikia sasa wanaoficha sukari, takwimu za wizara ya kilimo zinaeleza, nchini hakuna sukari ya kutosha lakini watu wanashughulika na kuitafuta sukari’
‘Pamoja na msako mkali sukari iliyokamatwa nchi nzima haifiki tani 10000 lakini kwa kuwa Rais ameshasema sukari imefichwa viongozi nao wanarudia kauli hiyo kuwa sukari imefichwa yasije yakawakuta yaliyomsibu mama Anne Kilango Malecela.
0 comments:
Post a Comment