Serikali imetakiwa kupigilia msumari sheria yake ya matumizi ya mtandao ili kuwadhibiti watu wanaotumia vibaya Teknolojia hiyo kwa kukiuka haki za msingi za Binadamu nchini Tanzania na watakao bainika iwachukulie hatua kali za kisheria badala ya kufumbia macho watu wanaoenda kinyume na matakwa ya mtandao.
Mashirika yanayotetea haki za binadamu hususani makundi maalum yamesema kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii yanaogofya ambapo bado wapo watu wanaotuma picha chafu na mbaya zisizofaa kwenye mitandao hiyo jambo ambalo linafanya udhalilishaji mkubwa na uvunjwaji wa haki za binadamu.
Kauli hiyo imetolewa muda mfupi na Mashirika yanayotetea haki za binadamu hususani makundi maalum kama watoto na wanawake mara baada ya kukutana na waandishi wa habari kulaani baadhi ya matukio mabaya yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na na kusisitiza kuwa sasa serikali ichukue hatua za haraka kudhibiti hali hiyo kwani inakwenda kinyume na sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya mtandao.
Bi HELLEN KIJO BISIMBA ni Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC ambao waliyaongoza mashirika hayo katika kutoa tamko hilo ambapo ameeleza kuwa katika kipindi cha karibuni kumekuwa na wimbi kubwa katika jamii kusambaza na kutumiana picha za watu waliofanyiwa ukatili,au waliopata ajali zikionyesha majeraha,au hata maiti za watu hao na zile ambazo zinaonyesha ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku serikali ikiwa haifwatilii swala hilo.
Unaweza ukasoma zaidi Mikakati mikuu katika hili.BOFYA HAPA->http://bit.ly/1WuQGTI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment