Kiongozi
wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema azindua kampeni za chama
chake na kuahidi kuwaokoa wananchi kutokana na umaskini, ukosefu wa
ajira na serikali ya ufisadi.
Takriban watu 40,000 walihudhuria
mkutano huo ulioandaliwa katika uwanja wa Soweto ambapo Malema alitoa
ahadi ya kuwarudishia ardhi iliyonyakuliwa na wazungu na pia kutaifisha
mabenkii.
Aidha Malema alibainisha kuwa uamuzi wake kuhusu kuchukua
ardhi kutoka kwa watu weupe si ubaguzi bali ni haki ya wananchi weusi wa
Afrika Kusini walionyanyaswa .
Aliendelea kueleza kuwa azimio lake ni kuona uswa baina ya jamii za weusi na weupe katika masuala ya ugawaji ya raslimali.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment