Image
Image

Manula:Sikukosea AZAM FC ndio sehemu sahihi kwangu kuinua kiwango changu cha Soka.

KIPA chaguo la kwanza wa Azam FC, Aishi Manula amesema kuwa anaishukuru klabu hiyo kwa kuchangia kuinua kiwango chake na kuwa mmoja wa magolikipa tegemeo nchini kwa sasa.

Manula ambaye yupo na kikosi cha Timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo jana ilicheza na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya alisema kuwa ubora wake uwanjani umetokana na klabu hiyo kumuamini na kumpa nafasi ya kucheza.
“Nafikiri kama isingekuwa klabu yangu ya Azam, labda nisingekuwa kwenye ubora huu, Azam imesaidia kukuza kipaji changu na kwa kweli najivunia kuwa kwenye klabu hii,” alisema Manula.
Alisema kuwa uwendeshwaji wa klabu hiyo unatoa fursa kwa wachezaji kujituma na kupandisha uwezo wao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment