Image
Image

MKAPA:Suala la amani ya Burundi lipo mikononi mwa Warundi wenyewe.

RAIS mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa amesema suala la amani ya Burundi lipo mikononi mwa Warundi wenyewe na kutaka pande zote zinazoshiriki kutafuta suluhu kuzungumza na kuondoa tofauti zao na kurejesha hali ya amani nchini mwao.
Mkapa aliyasema hayo jana wakati akifungua mjadiliano ya kutafuta amani Burundi yaliyoanza jana jijini Arusha.
Alisema yeye kama msuluhishi ni kiungo tu cha kuwezesha Warundi kwa uwakilishi wa wadau wote kuzungumza na kupatana kuweka amani katika taifa lao.
“Sote tunafahamu kuwa jukumu langu hapa ni kuwaunganisha tu mpate fursa ya kuzungumza na kukubaliana kwa sababau tatizo hapa ni la nchi yenu na ninyi ndio mtakaokubaliana,”alisema Mkapa katika hotuba yake.
Alisema atahakikisha kuwa anatoa muda wa kutosha kwa wadau wote kutoa maoni yao juu ya mustakabili wa suluhu ya Burundi.
“Natoa mwito wakuu wa nchi ya Burundi, vyama vyote vya siasa, taasisi za kidini na wanasiasa maarufu, wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika suala hili,”alisema.
Aliongeza kuwa kabla ya mazungumzo hayo kuanza alifanya mashauriano na wakuu wa nchi wanachama wa Afrika mashariki, Umoja wa Afrika (AU) ili kupata mawazo yanamna bora ya kushughulikia suala la amani ya Burundi.
Alisema anatambua mchango mkubwa wa Jumuiya ya Kimataifa, Jumuiya ya Afrika Mashariki katika usuluhishi wa Burundi.

Akizungumza katiak ufunguzi wa majadiliano hayo, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Balozi Jamal Benomaar, alisema Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kila mara limekuwa likona hali mbaya ya amani nchini Burundi na hivyo kwa mara nyingine linasisitiza pande zinazosigana katika mgogoro kuzungumza na kurejesha amani nchini humo.
“Ni pale pande zote zitakapofanya jambo hilo kwa moyo na kwa dhati ndiyo tatizo la mgogoro wa Burundi itakwisha, wakumbuke kuwa kile kinachoendelea nchini mwao itakuwa juu yao,”alisema.
Alisema Umoja wa Mataifa umetoa msaada kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kusuluhisha mgogoro wa Burundi na kufurahia kuteuliwa kwa Rais Mkapa kusuluhisha mgogogro huo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Liberat Mfumekeko, alisema kuwa Jumuiya hiyo inafanya kazi na msuluhishi ili kuhakikisha kuwa lengo la kupatikana kwa amani nchini Burundi linafikiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment