Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Ramadhani Diliwa (katikati).
WATUMISHI watano wa halmashauri ya wilaya ya Handeni, wamefukuzwa kazi kutokana na utoro wa muda mrefu kazini bila maelezo yoyote kitu ambacho ni kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Tukio hilo lilitokea jana kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, kilichofanyika ukumbi wa halmashauri ambapo baada ya kikao maalum walitoka na azimio hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Ramadhani Diliwa, alisema Baraza limechukua hatua hizo kutokana na watumishi hao kutoonekana kwa muda mrefu kazini bila taarifa za kuridhisha kitu ambacho ni kinyume na sheria za utumishi wa umma.
Diliwa aliwataja watumishi waliofukuzwa kazi kuwa ni John Hongoa ambaye alikuwa ni Kaimu Ofisa Misitu, James Ivory (Tabibu),Washington Mbibo alikuwa Ofisa Mipango Msaidizi, Sosten Seiya (Tabibu) na Doreen Nyuso ambaye pia ni Tabibu.
Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za Jamii ambaye pia ni diwani wa kata ya Ndolwa, Joel Mabula alisema hatua hiyo itaendelea kwa kila baraza watakalokuwa wanakaa ili kuweka halmashauri sawa kwani kuna baadhi wa watumishi wamekuwa wakidharau mabaraza hayo.
Baraza hilo la pili la halmashauri ya Wilaya ya Handeni hadi sasa limesimamisha kazi wakuu wa idara watatu na mtendaji mmoja kutokana na shutuma mbalimbali za matuminzi mabaya ya ofisi ikiwemo kufukuza kazi wengine watano wakieleza lengo ni kutaka kuleta nidhamu katika utendaji.

0 comments:
Post a Comment