WAZIRI wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alifanikiwa kukonga nyoyo za wabunge wengi baada ya kufafanua kwa kina mikakati kadhaa itakayoiwezesha Tanzania kuwa na umeme wa kutosha hadi kuuza kwa nchi jirani Afrika Mashariki.
Muhongo aliyasema hayo wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17 bungeni mjini Dodoma juzi.
UZALISHAJI WA UMEME
Akielezea kuhusu uzalishaji wa umeme, Muhongo
Tanzania hivi sasa inajivunia kuwa na vyanzo vingi vya nishati hiyo na hivyo hakuna kubahatisha.
"Tanakokwenda hatubahatishi… hotuba yangu haina malalamiko, ina tarakimu na mahesabu," alisema kabla ya kuongeza: "Tunataka tuuze umeme nchi nzima kwa bei nafuu ya senti saba kwa unit. Tunataka tuuze pia Afrika Mashariki.”
Aidha, Muhongo alisema ili kufanikisha malengo yote hayo, Tanesco itaendelea kubadilika na kwamba, uuzaji na uzalishaji wa umeme sasa upo wazi kwa kila mtu.
MIKATABA MIBOVU IPTL, SONGAS
Akizungumzia mikataba iliyopo ambayo Tanesco imeingia na wabia mbalimbali katika kuzalisha na kusambaza umeme nchini, Prof. Muhongo alisema hakuna cha kuficha bali ni kutanguliza ukweli kuwa mikataba yote iliyoingiwa ni mibovu.
"Nakiri kuwa deni la Tanesco ni kubwa. Na hii inatokana na mikataba mibovu, ruswa na uongozi dhaifu. Na ndugu zangu Watanzania niwaeleze, mtu asije akawaeleza unafuu wa kampuni yoyote inayoiuzia umeme Tanesco sasa hivi, haipo. labda tu (mtu) awe ametumwa kuishabikia," alisema na kushangiliwa.
"Tutasema ukweli mbele ya Mwenyezi Mungu,. Mikataba yote si mizuri… sasa nimechukua hapa mifano, Songas tulikuwa tunalipa 'capacity charge' kwa mwezi dola za Marekani milioni 4.6, Symbion dola milioni 2.4, IPTL dola milioni 2.6, Aggreko dola milioni mbili. Nawaomba waheshimiwa wabunge, msitumike kuja hapa kuishabikia," alieleza zaidi Prof. Muhongo.
UMEME WA GESI
Kutokana na kuwapo kwa gesi ya asili, Prof. Muhongo alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kutoongeza mikataba na kampuni zinazozalisha umeme kwa kutumia mafuta kwa kuwa umeme wake ni wa bei ghali.
Aidha, alisema hivi sasa wameanzisha utaratibu wa kupima utendaji wa kila kampuni inayozalisha umeme nchini kila baada ya miezi mitatu na wasiotimiza malengo watakuwa wakiwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Katika hatua nyingine, serikali imetangaza kukizuia kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara kuagiza nje ya nchi makaa ya mawe kwa ajili ya uzalishaji wa saruji na badala yake kugeukia makaa yaliyopo nchini.
Kuhusiana na mafuta, Prof. Muhongo alisema ili kudhibiti ufisadi katika kugawa maeneo yenye mafuta, serikali imeamua kulitoa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika utafutaji wa mafuta.
"Sasa tumeanzisha chombo kingine kinachoitwa PURA ambacho kitaisimamia hata TPDC yenyewe ili kuleta ufanisi katika utendaji," alisema.
BAJETI YA WIZARA
Ili kutekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedha 2016/17, serikali imetenga jumla ya Sh. trilioni 1,123 kwa ajili ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, huku Sh. trilioni 1,056 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo, sawa na asilimia 94 ya bajeti yote ya wizara hiyo.

0 comments:
Post a Comment