Image
Image

Mwalimu wa kike achapwa’ makofi na mwalimu wa kiume mbele ya wanafunzi.


MWALIMU Fatma Ramadhani wa Shule ya Msingi Amani, Kata ya Nyarugusu wilayani Geita, amegoma kuingia darasani baada ya ‘kuzabwa’ makofi na mwalimu wa kiume mbele ya wanafunzi.

Mwalimu anayedaiwa kumzaba mwenzake ni Mohamed Khatibu, ambaye baada ya tukio hilo, Fatima aliangua kilio mbele ya wanafunzi wake.
Fatma alisema tukio hilo linatokana na visa vingi vya unyanyasaji wa kijinsia anavyofanyiwa na mwalimu huyo ukiwamo wa kumtaka kimapenzi kwa kutumia fursa ya kuwapo walimu 14, huku wakike akiwa peke yake.
Akitokwa na machozi, mwalimu huyo alisema baada ya tukio hilo alishinikizwa na walimu wengine akiwamo Mwalimu Mkuu, Rajab Besa, kutaka suala hilo kulimaliza kinyemela bila ya kulifikisha kwenye vyombo vya sheria huku akibembelezwa kwa kupatiwa Sh. 70,000 kati ya 130,000 alizoahidiwa kupewa na mtuhumiwa ili aweze kupatiwa matibabu chini ya usimamizi wa mwalimu mkuu.
Alidai, alitishwa na walimu wenzake iwapo atachukua hatua ya kushitaki, hatapewa ushirikiano wa kutoa ushahidi zaidi ya kujikuta matatani hivyo kupoteza kazi.
“Ugeni wangu katika ajira hii, umenifanya nishindwe kufahamu wapi naweza kupata haki yangu, kutokana na walimu wezangu kutonipa ushirikiano hivyo kutumia nafasi hiyo kuninyanyasa,” alisema.
Alisema tukio hilo si la kwanza, kwani mwaka uliopita mwalimu mwingine wa kiume wa shule hiyo aliyekuwa akiishi naye nyumba moja, alimvunjia mlango wa chumba chake saa 5 usiku, lakini hakufanikiwa kutimiza lengo lake la ubakaji na suala hilo alitakiwa lisuluhishwe shuleni.
Alisema baada ya tukio hilo aliamua kuhamia kijiji kingine cha Nyarugusu na kumlazimu kutembea umbali mrefu wa kilometa zaidi ya sita kila siku kwenda shuleni.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Rajab Besa na ‘mtuhumiwa’ Khatibu, walikataa kuzungumzia tukio hilo kwa madai lipo kwa Ofisa Elimu Halmashauri ya wilaya.
Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Paschal Joseph, alisema siku ya tukio alikuwapo shuleni hapo katika ofisi ya mwalimu mkuu, lakini hawezi kuthibitisha kama mwalimu huyo alipigwa inagawa alimuona akitokwa na machozi na kuingia ofisi ya mwalimu mkuu.
“Mwalimu Fatma aliinga ofisi ya mwalimu mkuu akibubujikwa machozi na kuomba kitabu ili aende hospitali kupatiwa matibabu, lakini mambo mengi shuleni hapo yamekuwa yakifanyika na kumalizwa kimyakimya,” alisema Joseph.
Ofisa Elimu ya Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Deus Seif, alisema baada ya kufika shuleni hapo na kukutana na walimu, alikemea tabia hiyo na kumuagiza mwalimu mkuu kukaa na walimu wake kuzungumzia suala hilo.
Alisema kwa sasa anaandaa ripoti ya kumkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa wilaya aliyempa jukumu la kufuatilia taarifa hizo ili kujulikana hatma yake.
    Share on Google Plus

    Kuhusu TAMBARARE HALISI

    This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

    0 comments:

    Post a Comment