Image
Image

Mwanamke aliyekaa siku 6 baada ya kufukiwa na kifusi atolewa hai Nairobi nchini Kenya.

Mwanamke ametolewa akiwa hai kutoka kwenye vifusi siku sita baada ya jumba kuporomoka katika mtaa wa Huruma, Nairobi.
Juhudi za uokoaji ba
do zinaendelea ingawa kuna wasiwasi kwamba muda wa kupata manusura wakiwa hai unayoyoma.
Kwa mujibu wa Pius Masai, mkuu wa kitengo cha taifa cha kukabiliana na majanga, idadi ya waliofariki kufikia sasa imefikia 36.
Watu 136 wameokolewa wa
kiwa hai lakini watu 70 kufikia sasa bado hawajulikani walipo.
Siku mbili zilizopita, mtoto wa umri wa miezi sita aliokolewa baada ya kukaa kwenye vifusi kwa siku nne.
Msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kupelekwa hospitalini.
Alipatikana akiwa amef
unikwa kwa blanketi ndani ya ndoo na hakuonekana akiwa na majeraha yoyote.
Babake mtoto huyo, Bw Ralson Wasike, akihutubia wanahabari baadaye, alisema bintiye amekuwa na nguvu sana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment