Wabunge
nchini Kenya wanatarajiwa kupiga kura, kwa mara nyingine, ya kupitisha
ama kupinga mswada wa sheria kuhusu usawa wa jinsia katika nyadhifa za
uteuzi na siasa.
Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya, nyadhifa zote za
uteuzi na uchaguzi katika afisi za umma hazifai kuchukuliwa na zaidi ya
theluthi mbili ya jinsia moja, iwe wanawake ama wanaume.
Mswada huo
ulihitaji wabunge kuungwa mkono na wabunge 233 ndipo uidhinishwe lakini
idadi ya wabunge waliohudhuria kikao, yenyewe haikufikia kiwango hicho.
Baada ya kura kupigwa, wabunge 179 waliunga mkono mswada huo, 16 wakapinga na 5 wakakosa kutangaza msimamo wao.
Wiki
iliyopita mswada huo ulifeli ambapo ni wabunge 195 pekee waliouunga
mkono, 28 wakaupinga, wawili wakakosa kutangaza msimamo wao huku 24
wakikataa kupiga kura.
Mwenyekiti wa muungano wa wabunge wanawake
nchini Kenya Cecily Mbarire alikuwa awali ameeleza matumaini kwamba
mswada huo ungeidhinishwa lakini hilo halikuwa.
"Tuna matumaini kuwa
mswada huu utaptishwa hivi leo, tumekuwa tukizungumza na wenzetu
wanaume, na kuwarai kutuunga mkono, na tuna matumaini,” alisema awali.
Kura
ya leo ilipigwa siku ya mwisho kabla ya wabunge kwenda likizoni, na kwa
kawaida kikao kama hicho huhudhuriwa na wabunge wachache.
Wabunge wanatarajiwa kwenda likizo ya mwezi mmoja baada ya kikao cha leo alasiri.
Rais
Uhuru Kenyatta, ambaye ni kiongozi wa muungano wa Jubilee, ulio na
wanachama wengi bungeni, alikuwa amewaomba wabunge kupitisha mswada huo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga pia alitoa ombi sawa na hilo kwa wabunge wa muungano wake wa CORD.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013, wanawake hawakuchaguliwa katika nyadhifa za ugavana na useneta.
Kati ya wabunge 290 waliochaguliwa na wananchi mwaka 2013, asilimia 5.5 pekee ya wanawake ndio waliochaguliwa.
Kati ya wawakilishi wa wodi 1450, ni wanawake 88 pekee waliochaguliwa.
Bunge
la kenya linajumuisha wabunge 290 waliochaguliwa na wananchi, wabunge
47 wanawake waliochaguliwa na wananchi kuwakilisha kaunti 47, na wabunge
12 maalum walioteuliwa na vyama vya kisiasa na spika wa bunge.
Home
Kimataifa
Kenya wanatarajiwa kupiga kura kupitisha ama kupinga mswada wa sheria kuhusu usawa wa jinsia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment