Image
Image

Ndege ya Misri yaanguka ikiwa na watu 66 katika bahari ya Mediterrania.

Ndege hiyo ilitoweka na kutoonekana tena kwenye mtambo wa rada dakika 45 kabla ya muda kamili ambao ilitarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Cairo. 
Maafisa nchini Misri wanasema ndege hiyo ilianguka saa nane usiku.
Maafisa nchini Misri wamesema kuwa ndege ya taifa hilo iliyokuwa ikisafiri kutoka Paris Ufaransa kuelekea Cairo imetoweka na huenda imeanguka katika bahari ya Mediterrania. Ndege hiyo ya shirika la EgyptAir ilikuwa na jumla ya watu 66 miongoni mwao wahudumu wa ndege hiyo. Shughuli za kutafuta mabaki ya ndege na manusura imeanzishwa.
Ndege hiyo ilitoweka na kutoonekana tena kwenye mtambo wa rada dakika 45 kabla ya muda kamili ambao ilitarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Cairo. Maafisa nchini Misri wanasema ndege hiyo ilianguka mwendo wa saa nane usiku majira ya Misri, jumla ya saa tatu na nusu tangu kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris. Hii ni muda mfupi baada ya ndege hiyo kutoweka na kutoonekana tena kwenye mtambo wa rada maili kumi ndani ya anga ya Misri.
Sababu ya kutoweka ni gani?
Chanzo cha ndege hiyo kuanguka hakijabainika. Awali kulitokea ripoti kwamba idara ya jeshi la Misri ilipokea taarifa ya kuonyesha kuwa ndege hiyo ilikumbwa na hali ya dharura. Lakini baadaye maafisa wamesema hakukuwa na wito wa dharura kutoka kwa ndege hiyo. Hali ambayo imeibua mkanganyiko. Waziri mkuu wa Misri Sherif Ismail alipoulizwa uwezekano wa njama ya kigaidi katika mkasa huo amejibu kuwa hawapuuzilii sababu yoyote inayoweza kukisiwa kusababisha ndege hiyo kuanguka.
"Kile tunachoweza kusema kwa sasa ni kuwa tulipoteza mawasiliano kwa saa fulani na sasa tunatafuta eneo hili… jeshi limetangaza kuwa lilipokea ishara wala si wito wa dharura lakini hiyo pia inachunguzwa na kuna idara za jeshi na wanajeshi wa majini wanapekua kila eneo kwa ushirkiano na Wagiriki, zipo ndege za Ugiriki zimehusishwa kwenye msako… hatuwezi kuthibitisha au kukana chochocte kwa wakati huu kuwa ndicho kimesababisha, hadi uchunguzi dhidi ya suala ukamilike tunaweza kusema hali ni nini?"
Kwa sasa vikosi vya usalama vya Misri vikishirikiana na vikosi kutoka Ugiriki vinaendeleza shughuli za kutafuta manusura, ndege hiyo au mabaki yake katika bahari ya Mediterania. Jamaa za abiria waliokuwemo ndani ya ndege wamefika katika uwanja wa ndege wa Cairo wakisubiri habari zaidi kuhusu wapendwa wao. Miongoni mwa waliokuwemo ndani ya ndege hiyo aina ya MS804 ni raia 30 wa Misri, wafaransa 15, wairaqi 2, watoto wawili na mmoja mdogo, Uingereza, Kuwait, Ubelgiji, Saudi Arabia, Sudan, Chad, Ureno, Algeria na Canada wakiwa na raia mmoja mmoja.
Kulingana na shirika la ndege hiyo, nahodha wa ndege kwa jina Said Ali Shaqir ana tajriba ya kuendesha ndege kwa zaidi ya saa elfu sita, na miongoni mwa ndege hizo 2000 zikiwa kubwa aina ya Airbus.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment