Image
Image

UHABA WA SUKARI:Upinzani wambana Waziri mkuu kutaka ufafanuzi.

  Kiongozi mkuu  wa kambi ya upinzani Bungeni Mh.Freeman Mbowe.
Na.Semvua Msangi.
Kutokana na uhaba wa Sukari ambao unaonesha kuchangia kupanda kwa bidhaa hiyo  hapa nchini Serikali imesema kwamba  mpango wake wa kutoa bei dira ya uuzwaji wa bidhaa hiyo ni kutokana wao serikali kukaa pamoja na wazalishaji wa viwanda vya sukari na kufanya mapitio nakufahamu bei wanayonunulia nchini Brazili na Uarabuni na kubaini kwamba mpaka inaingia nchini inafaa kuuzwa kwa bei hiyo elekezi.
“Mpaka Sukari inaingia nchini na kulipa kodi na usafirishaji kutoka Dar es Salaam mpaka kagera,Lindi na Ngara tunafahamu itauzwa beigani wajibu wa Serikali wa kutoa bei dira nikumlinda mwananchi wa kawaida asije kuuziwa kwa gharama kubwa kwa kisingizio cha usafirishaji huku tukiwa tunajua usafirishaji kutoka Brazili na Uarabuni unakuwaje”Alisema Majaliwa.
Kiongozi mkuu  wa kambi ya upinzani Bungeni Mh.Freeman Mbowe ameuliza swali moja lenye vipengele viwili kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati wa Maswali na Majibu akitaka kufahamu kwamba 1.Pamoja na nianjema sana ya kulinda viwanda vya ndani nidhahiri kwamba maamuzi yote ya kiutawala lazima yafanyiwe kwanza utafiti na tunapozungumza Mh.Waziri Mkuu nna hakika Serikali yako inatambua kwamba kuna mradi mkubwa wa uwekezaji wa kiwanda cha Sukari uliokuwa umependekezwa katika eneo la Bagamoyo uliozungumza ambao umeanza kuratibiwa tongu mwaka 2006 wenye Capacity ya kuzalisha Sukari Tani laki moja na elifu ishirini na tano kwa Mwaka lakini Serikali mpaka dakika hii tunapozungumza urasimu wa mradi huuhaujapewa kibali cha kuanza.
2. Waziri Mkuu pamoja na kwamba ulisema kuna bei elekezi ya Sukari ambayo ingehitaji soko la sukari liweze kuwa Control na Serikali jambo ambalo linaonesha kushindikana unatupa kauli gani watanzania kuhusiana na hayo mambo niliyokuuliza?.
Waziri Mkuu Majaliwa akijibu Swali hilo la kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Mh.Freeman Mbowe amesema kwamba Shamba la Bagamoyo kwa ukubwa na mategemeo yake  kwa mipango ya kuzalisha sukari inategemea sana mto wami,Mpakani Mwa mto wami umepakana na mbuga ya Sadani.
“Mbuga ya Sadani uwepo wake na sifa iliyonayo inategemea sana wanyama wale wa kunywa maji mto wami,uwekezaji wa Shamba la Sukari unahitaji Maji mengi na haya yanatakiwa yatoke mto wami.”Alisema Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema bado kuna mgongano wa mpaka kati ya shamba hilo la Sukari linalotegemewa kulima miwa na mbuga ya Sadani, Kamati ya kudumu ya Bunge imefanya ziara na kuishauri Serikali kuangalia vinginevyo.
“Na mimi nimepokea ushauri wao kwa kuona kwamba una mantiki,Kamati ya Bunge imeshauri Serikali kwamba nivyema tukahifadhi mbuga tukatafuta maeneo mengine ya Kilimo cha Sukari ili kulinda mto wami unao tumiwa na wanyama wetu kwenye mbuga ya sadani,na sisi tunanafasi kubwa ya maeneo mengi ambayo yamefanyiwa utafiti wa kulima Sukari.”Amesema Majalia.
Pia amesema kwamba mbali ya eneo la Kilogoro na Kigoma bado Serikali ina shamba lililokuwa likimilikiwa na Bodi ya Sukari katika eneo la Kilombero ambalo linanafasi nzuri  hivyo wataenda kufanya mazungumzo na wakulima wanaolima mashamba ya kawaida wawaachie ili waweze kuwekeza.
Amesema kuwa upo mto Rufiji na Bonde kubwa llililokuwa linamilikiwa na watu wa Bonde la Rubada,hivyo watakapo pata wawekezaji wengi wataanza kupima viwanda vilivyopo na uzalishaji wake, Makubaliano ya kiwanda kipya na uzalishaji wake na watakapo gundua kwamba mahitaji yake yanatosha mahitaji ya nchi wataanza kuwakabidhi Kigoma,Morogoro,Kilosa na Ngerengere kutokana na Kamati ya bunge kuwashauri vizuri juu ya kulinda Mbuga ya Sadani.
Hata hivyo Waziri mkuu akatolea ufafanuzi wa kina wa Bei elekezi ya Sukari na kusema kuwa bei hiyo lengo kuu ni kumlinda mlaji ama mwananchi wa kawaida lakini endapo kutakuwa na mabadiliko atayweza kuyazungumza.
“Swala la bei elekezi litategemea linaweza likabadilika kutegemea na gharama ya usafirishaji ambayo na sisi pia tunafuatilia kwa ukaribu kupitia bodi yetu ya Sukari,hivyo swala la bei dira linaweza kubadilika na sitotoa kauli kutegemea na uagizaji lakini wananchi waamini kwamba Serikali hii inawalinda walaji wadogo wasinunue sukari kwa bei ya juu.”Amesema Majaliwa.   
Aidha kwa sasa katika baadhi ya maeneo Sukari imeendelea kupaa kwa bei ya juu huku Mwanza - 6000/, Arusha 4000, Kiteto 4000, Songea 3500,Dar es Salaam 3200 na Mbeya 3000 ,huku bei elekezi ya Serikali ikitaka wauzaji wauze Kilo moja ya Sukari shilingi 1800/=

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment