Mshambuliaji
wa Cameroon Samuel Eto’o anayechezea kilabu ya Antalyaspor nchini
Uturuki, anaendelea kujijengea sifa kwenye ligi kuu ya soka ya Super Lig
Spor Toto.
Eto’o ameonyesha umahiri wake kwa kufungia Antalyaspor jumla ya magoli 20 kwenye ligi katika mechi 31 zilizochezwa.
Kufuatia
mafanikio hayo, Eto’o anaendelea kukimbizana na mshambuliaji wa
Ujerumani Mario Gomez anayechezea kilabu ya Beşiktaş na ambaye kwa sasa
amefunga jumla ya magoli 24.
Msemaji wa kilabu ya Antalyaspor Hasan
Ali Ceylan alibainisha umuhimu wa Samuel Eto’o kwenye timu hiyo na
mchango wake mkubwa alioleta katika mafanikio yao.
Vile vile, Ceylan
pia alifahamisha kwamba mchezaji huyo atapokea malipo ya ziada kufuatia
makubaliano yao ya mkataba kwa kuifungia magoli 20.
Home
MICHEZO
Slider
Nyota wa Cameroon Samuel Eto’o akimbizana na Mario Gomez kwenye kinyang’anyiro cha mfungaji bora.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment