Waziri
wa mazingira wa Tanzania Januari Makamba, amesema asilimia 61 ya eneo
la nchi hiyo liko hatarini kuwa jangwa kwa sababu ya uharibifu mkubwa wa
mazingira unaoendelea.
Akiongea kwenye kikao cha bunge mjini Dodoma
amesema nchi hiyo inapoteza wastani wa ekari milioni moja za misitu kwa
mwaka, na kwamba katika muongo uliopita eneo lililopotea ni sawa na
ukubwa wa nchi jirani ya Rwanda. Amefafanua kuwa tatizo hilo
linasababishwa sana na mahitaji makubwa ya bidhaa zinazotokana na miti
zikiwa kama chanzo cha nishati, na amebainisha kuwa asilimia 90 ya
nishati hiyo inatokana na misitu.
Aidha amesema wimbi la uharibifu wa mazingira pia linaathiri vyanzo vya maji na maeneo ya vyanzo hivyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment