Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika limetoa wito wa kukamatwa kwa maafisa wa polisi waliohusika katika kuwapiga wafuasi wa CORD waliokuwa wanaandamana hapo jana.
Hii ni baada ya kijana aliyeonekana akipokea kipigo kutoka kwa maafisa wa polisi kuripotiwa kuaga dunia mapema leo.
Katika taarifa yake aliyoituma katika chumba chetu cha habari,mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Hussein Khallid amesema ni jukumu la polisi kuhakikisha kuwa kuna usalama na sheria zimezingatiwa lakini sheria haijawapatia ruhusa ya kutumia nguvu kupita kiasi.
Khalid Amekemea vikali ghasia zilizoshuhudiwa hapo jana na amesema ukiukaji wa haki ni lazima uishe humu nchini kwa kuanza kuwachukulia hatua polisi waliohusika.
Hapo jana baadhi ya wafuasi wa chama cha ODM kwenye kaunti ya Kisumu na Nairobi walijeruhiwa kwenye maandamano ya kutaka kubanduliwa kwa makamishena katika tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini kabla ya uchaguzi mkuu ujao yanayoongozwa na mrengo wa CORD.
0 comments:
Post a Comment