Mbunge Kigoma Kusini Hasna Mwilima kupitia tiketi ya CCM ameshinda kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na David Kafulila (NCCR-Mageuzi) Korti Kuu Kanda ya Tabora.
Mahakama hiyo imesema Kafulila na mashahidi wake wameshindwa kuthibitisha madai kwamba alimshinda mpinzani wake, hivyo Mwilima ndiye mshindi halali.
Hata hivyo, Kafulila amesema hakubaliana na hukumu hiyo na kuahidi kukata rufaa, jambo linaloungwa mkono na wafuasi wa chama chake na Ukawa kwa ujumla.
Wafuasi wa CCM wamefurahia hukumu hiyo wakisema Mahamaka Kuu Kanda ya Tabora imetenda haki kwa kumpa ushindi Mwilima.
Baada ya hukumu hiyo, Mwilima amesema nguvu zake sasa anaelekeza kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo lake.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment