Image
Image

Tusipuuze Mapambano dhidi ya kipindupindu yawe ya kudumu

HIVI karibuni vyombo vya habari vilieleza kuwa serikali imeamua kutoa taarifa ya ugonjwa wa kipindupindu kila wiki. Kwa mujibu wa habari hiyo, serikali iliamua kuanzisha utaratibu huo, kwa lengo la kuhabarisha Watanzania kuhusu juhudi zinazofanywa na mikoa na wilaya nchini kukabiliana na ugonjwa huo.
Tunampongeza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa kutangaza hatua hiyo, ambayo imesaidia mno kufahamisha wananchi kuhusu ugonjwa ulivyo nchini na kwa hakika utoaji taarifa huo, umekuwa endelevu.
Tunatoa rai kwa wakuu wa mikoa na wilaya, kuhakikisha kuwa wanaendelea kupeleka taarifa sahihi makao makuu ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam, za watu walioathirika na ugonjwa huo. Tunaonya kuwa kuficha taarifa za ugonjwa huo, hakutasaidia, kwa kuwa utaendelea kusambaa katika maeneo mengine nchini.
Tunaomba wizara hiyo ya Afya, iendelee kushirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali, hasa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Elimu ya Sayansi, Teknolojia na Ufundi, ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya kupambana na ugonjwa huo.
Tunahimiza Watanzania wote, kuacha kufanya mchezo wa ugonjwa huo, kwani ni hatari na wenye madhara makubwa. Hadi sasa ugonjwa huo umeshaua watu wengi na pia kusababisha wengi kulazwa hospitalini. Mathalani, watu waliougua ugonjwa huo ni zaidi 20,000 nchini na waliokufa ni zaidi ya 200.
Ugonjwa huo ulizuka Dar es Salaam na hadi mwanzoni mwa mwaka huu, ulikuwa umekwishasambaa katika wilaya 46 na mikoa 21 ya Tanzania Bara. Mikoa iliyowahi kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ni pamoja na Morogoro, Mara, Arusha, Singida, Mwanza na Manyara.
Lakini, kwa namna ya kipekee, tunatoa pongezi kwa mikoa ya Kilimanjaro na Iringa, ambayo katika kipindi kirefu haikuwa na taarifa za ugonjwa huo. Tunapongeza wakuu wa mikoa na wilaya za mikoa hiyo miwili kwa juhudi kubwa, walizofanya kudhibiti ugonjwa huo hatari.
Aidha, tunaipongeza mikoa ya Shinyanga, Pwani na Kagera, ambayo nayo haikuathiriwa mno na ugonjwa. Tunaomba wadau wengine, kama vile makampuni ya simu za mkononi, kushirikiana na serikali katika mapambano ya kutokomeza ugonjwa huo.
Tunasema hivyo kutokana na ukweli kuwa hadi sasa Watanzania zaidi ya milioni 10, wanatumia mitandao ya simu. Makampuni hayo ya simu, yanaweza kutumia teknolojia yao kufikisha kwa haraka na kwa wananchi wengi elimu ya kupambana na kipindupindu, kama vile dalili za ugonjwa huo, jinsi ya kuutibu na mbinu za kuzuia usisambae.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment