Image
Image

Polisi wawatia mbaroni wamiliki wa danguro, kaka na dada poa Dar

WAMILIKI sita wa madanguro na wauza miili yao maarufu kama kaka na dada poa, wametiwa mbaroni jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, aliwataja wamiliki wa madanguro hayo wanaoshikiliwa polisi kuwa ni Chiku Msafiri, Diula Victor, Ally Mwinyimvua, Shellen Newe, Mrisho Khalfan na Zaina Mussa, wote wakazi wa Temeke.
“Mei 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilifanya operesheni ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali maeneo ya Temeke na kufanikiwa kukamata wamiliki sita wa madanguro na wafanyabiashara wa kuuza mili yao kaka na dada poa,” alifafanua Kamanda Sirro.
Aidha, Kamanda Siro amewaonya wamiliki wote wa madanguro ikiwa ni pamoja na kaka na dada poa, kuacha mara moja biashara hiyo kwani ni kinyume cha sheria na watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment