Watu wawili wasio fahamika mara moja wamemuuwa kwa kumpiga risasi Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Makao Makuu Dar es salaam, Sajenti Ally Kinyogoli usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake eneo la Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga amesema kuwa watu waliomuuwa Marehemu kinyogoli walikwenda nyumbani kwakwe wakiwa na usafiri wa Pikipiki aina ya Boxer, na ndipo walipofika nyumbani hapo wakagonga mlango kisha wakatoka watoto na ndipo wakawaagiza wakamwite baba yao na baada ya kutoka tu ndipo wakamshambulia kwa kumpiga risasi tatu sehemu za mwili wake ikiwamo Mbavuni,Mkononi na kichwani .
Hata hivyo mara baada ya kufanya tukio hilo hawakuondoka na kitu chochote dhidi ya kukatika maisha ya Askari huyo wa usalama Barabarani Sajenti Kinyogoli na kisha kutokomea kusiko julikana,ambapo pia Polisi wapo katika hatua za kuwatafuta watu hao.
Kamanda Kinyogoli Enzi za uhai wake alifahamika zaidi Kupitia Kipindi cha Usalama Barabarani ambacho kimekuwa kikirushwa na Radio One Kila asubuhi,na Jioni lengo kuu la kipindi hicho ilikuwa nikufahamu hali ilivyo katika barabara mbalimbali za jiji la Dar es Salaam lenye Wingi mkubwa wawatu, ilikuwajuza endapo kutakuwa na eneo njia haipitiki ama kuna tatizo basi wapitie njia gani kwenda kazini ama kurudi kazini.
Mpinga amesema kwamba katika enzi zauhai wa Marehemu Kinyogoli hakuwahi kumueleza kuwa alikuwa na mgogo wa aina yeyote na mtu wala kwamba kulikuwa na mtu anamfuatilia kwa kitu chochote,Mazishi yake yatafanyika leo saa kumi maeneo ya Ukonga Mzambarauni.
Mpinga athibitisha kifo cha Kinyogoli,Video kwa hisani ya ITV Nimekuwekea hapa.
Mazishi ya marehemu Kinyogoli yanafanyika leo Sakumi Ukonga Mzambarauni,Video nimekuwekea hapa
0 comments:
Post a Comment