Image
Image

Serikali kutafakari kwa kina ombi la walemavu kuongezewa muda wa kustaafu.

Serikali imesema bado inatafakari ombi la watu wenye ulemavu la kuwaongezea muda wa kustaafu kutokana na wengi wao kuchelewa kuanza shule kutokana na hali ambayo wanayo.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu –sera ,bunge, kazi, ajira,vijana na watu wenye ulemavu Dr.Abdalah Possi amesema hayo bungeni mkoani Dodoma.
Amesema mara baada ya yeye kuchaguliwa kuwa naibu waziri ofisi ya waziri mkuu alikutana na makundi ya watu wenye ulemavu na kujadiliana nao mambo mbalimbali yanayowahusu likiwemo hilo.
Awali bungeni hapo Mbunge wa viti maalum, Dr.Elly Macha aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwapa walemavu upendeleo katika umri wa kustaafu kwa kuwa wengi wao huchelewa kuanza shule sambamba na kuanza kazi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment