Image
Image

Serikali yaongeza bajeti ya umeme wa REA kwa Asilimia 50 vijijini.

Serikali imeongeza bajeti ya maendeleo kwa Wakala wa Umeme Vijijini -REA kwa asilimia 50 ili kuhakikisha maeneo ya vijijini yanapata huduma ya umeme kama ilivyokusudiwa.
Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Waziri Muhongo amesema mradi wa umeme vijijini unatekelezwa kwa kasi na kusema serikali imeamua kuongeza fedha za maendeleo kwenye mradi huo.
Kwa upande wake Msemaji wa kambi rasmi ya upinzani bungeni juu ya Wizara ya Nishati na Madini John Mnyika amesema kuna kila sababu ya taifa kuhakikisha inawekeza katika miradi ya upatikanaji wa umeme.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment