Makamu
wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu amewataka
viongozi wa siasa na serikali kufuata taratibu za uwajibishwaji wa
watumishi pindi inapotokea kasoro katika utendaji wao.
Akizungumza na
Wauguzi na wananchi wa mkoa wa Geita katika siku ya wauguzi duniania
ambapo kitaifa imefanyika katika mkoa wa Geita Mama Samia amesema
serikali itaendelea kuboresha stahiki na mazingira ya kazi kila
itakapoweza ili kuwafanya watumishi wa umma kufanya kazi katika
mazingira bora.
Naye Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa
Mheshimiwa George Simbachawene amesema atasimamia na kuhakikisha haki za
wauguzi zinapatikana kwa wakati ili kuboresha huduma ya afya nchini.
Awali
akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Rais wa chama cha wauguzi Tanzania
Paul Magesa amesema mpaka sasa kuna uhaba wa wauguzi kwa asilimia
hamsini na moja tu jambo hili huwafanya wauguzi kufanyakazi nyingi
katika mazingira magumu hivyo kuomba ajira ziongezwe katika sekta hiyo.
Home
News
Slider
SAMIA: Watumbueni kwa kufuata taratibu na Sheria watumishi wenye kasoro katika utendaji.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment