Baraza
la maseneti nchini Brazil limeidhinisha kura ya kumfungulia mashitaka
rais Dilma Roussef ambapo sasa atapaswa kumuachia madaraka makamu wake
ili mchakato wa kushitakiwa uendelee.
Baraza la maseneti nchini
Brazil limeidhinisha kura ya kumfungulia mashitaka rais Dilma Roussef
ambapo sasa atapaswa kumuachia madaraka makamu wake ili mchakato wa
kushitakiwa uendelee.
Rais Dilma Roussef atakabidhi madaraka kwa
hasimu wake , makamu wa rais Michel Timer baada ya idadi kubwa ya
maseneta kujitokeza kumpigia kura ya kuidhinisha rais huyo kushitakiwa
katika mchakato ambao uliendelea usiku kucha wa kuamkia siku ya alhamis.
Idadi
kubwa ya wajumbe katika baraza lenye maseneta 81 ndiyo iliyohitajika
katika kupititisha maamuzi hayo ya kusimamisha kazi kwa miezi sita
wakati mchakato wa mashitaka ukiendelea. Makamu wa rais Temer atashika
wadhifa huo unaohitimisha miaka 13 ya utawala wa chama cha wafanyakazi
cha mrengo wa kushoto cha rais Roussef. Temer amesema anaandaa serikali
yake itakayojaribu kunusuru uchumi wa nchi hiyo uliodorora.
Ikiwa
imebaki miezi mitatu kabla ya kuanza kwa mashindano ya Olympic mjini Rio
de Janaiero, Brazil sasa inapambana kustawisha uchumi ulioporomoka
pamoja na kushughulikia kashfa za rushwa zilizokita mizizi kwa wanasiasa
na wafanyabiashara.
Awali mahakama ya juu nchini humo imeamuru
kufanyike uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi ya kiongozi wa upinzani
seneta Aecio Neves ambaye alikuwa mpinzani wa Bi. Roussef katika
uchaguzi wa mwaka 2014. Anatuhumiwa kwa utakatishaji wa fedha na
kuchukua hongo, ni miongoni mwa maseneta ambao wanaunga mkono suala la
kumshitaki rais.
Migogoro mingi iliyopo kwa sasa imeigawa nchi hiyo,
wapo ambao wanataka rais ashitakiwe, wengine bado wanaona kwamba chama
hicho kilichoko madarakani kimefanya kazi kubwa ya kuwaondolea umaskini
mamilioni ya raia.
Jitihada za rais huyo kuepukana na kikaango cha
kuondolewa madarakani , zilififia siku ya jumatano baada mahakama
kukataa ombi la mwanasheria mkuu la kubatilisha mchakato huo.
Seneta
Paulo Paim, mshirika wa rais Roussef anaona kuwa hakuna "muujiza" na
kwamba wanapambana kushinda. Magno malta , seneta kutoka chama cha
upinzani cha PR anasema kura hiyo ni sindano inayohitajika katika
kuiponya nchi.
Hata hivyo wapo wanaodhani kuwa hata kama Roussef
ataondolewa, matumaini ni madogo ya kupata maendeleo. Mmoja wa wananchi
anayeunga mkono kura hiyo Sulineide Rodrigues anasema kuwa na hapa
namnukuu "hatufikirii kwamba Temer atakuwa mzuri, ingawa "tutaendelea
kuwaondoa hadi hapo atakapopatikana yule anayewasikiliza wabrazil"
mwisho wa kunukuu.
Wakati kikao cha maseneta kikiendelea, kumekuwa na mapambano ya pande mbili katika miji ya Brasilia na Rio.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment