Marekani
imeahidi kuunga mkono mpango wa kanuni kadhaa zinazowapa mamlaka
wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na polisi kutumia nguvu
ili kuwalinda raia katika migogoro ya kivita.
Mpango huo umeungwa
mkono na Rwanda na Uholanzi. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa
Samantha Power ametoa tangazo hilo katika mkutano wa ngazi ya juu wa
Umoja wa Mataifa ulioangazia wajibu wa kuwalinda raia wanaokumbwa na
machafuko, akisema kuwa Marekani “inajivunia” kujiunga na mataifa
mengine 28 yaliyosaini mpango huo unaojulikana kana Kanuni za Kigali.
Walinda
amani kutoka nchi 29 katika operesheni zilizoidhnishwa na Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa kuwalinda raia sasa wanaruhusiwa kuchukua
“hatua ya moja kwa moja ya kijeshi dhidi ya makundi yenye silaha yenye
nia ya wazi ya kuwadhuru raia” – na makamanda wao wanaweza kuamuru
matumizi ya nguvu “katika hali ya dharura” bila kushauriana na wakuu
wao.
Power amesema Kanuni za Kigali zimetayarishwa kuhakikisha kuwa
raia hawatelekezwi tena na jamii ya kimataifa, akirejelea namna walinda
amani wa Umoja wa Mataifa walivyoondoka Rwanda kabla ya mauaji ya
halaiki ya mwaka wa 1994 na Srebrenica kabla ya mauaji ya kinyama ya
1995.
Simon Adams, mkurugenzi mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Wajibu
wa Kulinda, anasema 10 kati ya operesheni 16 za kulinda amani za Umoja
wa Mataifa, ikiwemo asilimia 97 ya wanajeshi 105,000 na polisi
wanaohudumu katika operesheni hizo, wana wajibu wa Baraza la Usalama
kuwalinda raia.
Hata hivyo, licha ya kuwapo kwa operesheni za kulinda
amani Umoja wa Mataifa unaendelea kupambana kuwalinda raia dhidi ya
makosa mengi ya kikatili katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo, Sudan
na Sudan Kusini. Anaongeza Adams.
Power alisema nchi 29 ambazo
zimeidhinisha Kanuni za Kigali zinajumuisha zaidi ya wanajeshi 40,000 wa
Umoja wa Mataifa na polisi, ikiwa ni zaidi ya thuluthi moja ya walinda
amani wa Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa ndio mchangiaji mkubwa wa
kifedha kwa operesheni za kulinda amani za umoja huo lakini una
wanajeshi wachache mno wanaotumwa katika operesheni zake.
Rwanda,
Uholanzi na Marekani ziliuanzisha mpango huo wa msingi ambao
uliidhinishwa katika mkutano wa ngazi ya juu mnamo Mei 2015 mjini Kigali
na mataifa makuu 30 yanayochangia wanajeshi na polisi kwa operesheni za
Umoja wa Mataifa, wachangiaji kumi wakuu wa kifedha namataifa mengine.
Waziri
wa Mambo ya Kigeni wa Uholanzi Bert Koenders aliumbia mkutano huo kuwa
watu na jamii zilizoko chini ya kitisho, bila mahali pa kwenda,
zinapaswa kujua kuwa Umoja wa Mataifa utafanya kila liwezekanalo ndani
ya uwezo wake kuwapa ulinzi.
Balozi wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa
Eugine-Richard Gasana alisema kanuni hizo zinaleta operesheni za
kulinda amani “katika karne ya 21”. Amesema zaidi ya wanajeshi 6,000 wa
Rwanda katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa wamepewa
mafunzo ya kuzingatia kanuni hizo na “wamejiandaa kutumia nguvu ikiwa
watahitajika” kwa ajili ya kuwalinda raia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment