Makamu
wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amesema
kuwa Serikali ya awamu ya tano itaanza kuwatumbua viongozi wa ngazi za
chini ambao wataisababishia Serikali upotevu wa mapato wakati wa
utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika bajeti ya Mwaka 2016 /17.
Kauli
hiyo ameitoa mjini Dodoma katika ufunguzi wa semina ya viongozi wa
chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma ambapo Mama Samia amesema kuwa
utumbuaji wa majipu hautakuwa kwa viongozi wa ngazi ya juu tu bali pia
utakuwepo kwa viongozi wa ngazi za chini.
Naye Mwenyekiti wa chama
cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewataka viongozi hao kwenda
kuisimamia serikali kutekeleza majukumu yake.
Kwa upande wake
,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Job Ndugai ambaye pia
ni mbunge wa Kongwa,ametaka kutungwa kwa Sheria ndogo ambayo itawapa
haki Sadiwani ya kuwawajibisha viongozi wanaotafuna mali za Umma.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment