Kwa upande wa Mkoa wa Tanga, takriban vyama vya ushirika 76, vimewasilishwa kwa mrajis wa vyama vya ushirika ikiwa ni mapendekezo ya kuvifuta kutokana na kushindwa kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza katika mahojiano na Nipashe Mrajis wa Mkoa wa Tanga, Jackline Senzighe, alisema vyama hivyo vimepewa kusudio la kufutwa kwa siku 90 yaani miezi mitatu ili kuhuisha uhai wa utendaji wao kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya vyama vya ushirika.
Idadi kubwa ya vyama hivyo imeelezwa kuwa ni vile vilivyoanzishwa wakati wa ahadi ya 'mabilioni ya JK' kwenye serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete.
Senzighe alisema vyama hivyo vilishindwa kuendesha shughuli zake kikamilifu huku baadhi vikionekana kuanzishwa kwa ushabiki wa kupata misaada.
“Wengi wao walianzisha vyama kipindi kile cha ahadi ya mabilioni ya JK wakitegemea fedha za msaada, matokeo yake wamekosa na vyama vimekufa, sasa hivyo ndiyo tunaendelea kuwahamasisha kuhuisha uhai ndani ya siku 90 kabla ya kuvifuta,”alifafanua Senzighe.
Alisema mkoa huo una jumla ya vyama vya ushirika 378 mpaka kufikia Desemba mwaka jana, huku vikiwa vimegawanyika katika makundi tofauti ikiwamo vyama vya ushirika vya mazao, uvuvi, viwanda, mifugo, umwagiliaji, madini, nyuki, vyama vikuu na Vyama vya Akiba vya Kuweka na Kukopa(Saccos).
Alisema vyama hivyo vilivyowekewa kusudio la kufutwa vimeshindwa kutimiza vigezo vya uhai wa chama ikiwamo kutokuwa na wanachama wa kutosha, kushindwa kufanyika kwa ukaguzi wa hesabu kwa muda mrefu, kutoitisha mikutano mikuu na kukosa uwezo wa kutoa michango na kutegemea misaada.
Kwa mujibu wa mrajis huyo wa Mkoa wa Tanga, ni kwamba vyama vya ushirika vyenye nguvu mkoani humo ni Saccos ambazo zinajumla ya wanachama 32,351 na mitaji ya Sh. bilioni 9.819.
“Saccos peke yake zipo 229 na zina nguvu sana, angalau kila wilaya kuna Saccos zinazoongoza kwa mkoa mzima, kwa hili tumefanikiwa changamoto ndiyo ipo kwa hivyo vyama vingine vya ushirika ambavyo kama vingeweza kufanya kazi zake vizuri vingekuwa ni vyanzo vizuri vya mapato kwa mwananchi mmoja mmoja na uchumi kwa mkoa kiujumla ,”alisema Senzighe.
Kutokana na hali hiyo, alivitaka vyama vya ushirika na wanachama wake kubadilika ili kuendana na mabadiliko ya ulimwengu wa kisasa yanayotawaliwa na uchumi unaotegemea nguvu za soko, utandawazi na teknolojia katika uzalishaji mali.

0 comments:
Post a Comment