Image
Image

Wananchi Ukerewe washauriwa kuzalisha mazao yanayoendana na mazingira ya hali ya hewa.

WANANCHI wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, wamshauriwa kuzalisha mazao yanayoendana na mazingira ya hali ya hewa badala ya kuendeleza kasumba ya kutegemea mihogo peke yake.

Wameshauriwa kuwa kwa kuendeleza kasumba hiyo, wanaweza kuathirika ikiwamo kukabiliana na tatizo la njaa.
Akizungumza katika ziara ya kukagua hali ya kilimo wilayani humo, Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Jumanne Mwasamila, alisema Ukerewe haina ukosefu wa chakula kwa kiasi kikubwa, bali wananchi wake wamekuwa wakitegemea ugali wa muhogo pekee kutokana na mazoea.
Mwasamila alisema zao la muhogo mara nyingi linakabiliwa na ugonjwa wa bandubandu na michirizi kahawia na kushambuliwa na wadudu wanaotishia kupotea kwa zao hilo.
Hata hivyo, mkurugenzi huyo alisema wakulima wengi kisiwani humo wameitikia wito wa kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi kama viazi vitamu, mahindi na mpunga ambayo yatasaidia kupunguza upungufu wa chakula kwa kiasi kikubwa.
Mpaka sasa hali ya chakula kilichotokana na mavuno ya shambani hadi kufikia Aprili, mwaka huu kuna tani 93,786.86 hivyo, kuwapo na upungufu wa tani 2,302.5 za chakula.
Naye Edwin Manuguliko mkazi wa kijiji cha Hamkoko katika Kata ya Ngoma wilayani humo, alisema baadhi ya wakulima wenzake wamekuwa wakikataa kufuata ushauri wa wataalamu na kufanya kilimo cha mazoea, hali ambayo inasababisha kuendelea kulima zao la muhogo.
    Share on Google Plus

    Kuhusu TAMBARARE HALISI

    This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

    0 comments:

    Post a Comment