Mbunge wa Viti Maalum, Kemilembe Lwota (CCM), alilifikisha suala hilo bungeni jana na kuitaka serikali itoe tamko kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika.
Kabla ya kuwasilishwa kwa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/17, Mbunge huyo aliomba mwongozo kwa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan, kutokana na kuwapo kwa video inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha udhalilishaji huo.
“Video hii inaonyesha udhalilishaji wa hali ya juu, utu na ubinadamu na ni kinyume cha mila za Kitanzania, Mwenyekiti naomba mwongozo wako. Naomba tamko la serikali hatua gani zimechukuliwa juu ya udhalilishaji wa mwanamke kwa wahusika,” alisema mbunge huyo.
Akitoa tamko la Serikali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema serikali imesikitishwa na tukio la binti wa Kitanzania kudhalilishwa.
“Ni udhalilishaji wa hali ya juu, kwanza amevuliwa nguo, kalazimishwa kufanya mapenzi na wanaume wawili na kurekodiwa tukio tukio kisha kusambazwa katika mitandao ya mbalimbali,” alisema Waziri Ummy.
Alisema yeye kama Waziri mwenye dhamana ya wanawake anakemea vikali tukio hilo na tayari amewasiliana na Waziri ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua.
“Hatua zimechukuliwa na tayari wahusika wamekamatwa na ni matumaini yangu watapelekwa mahakamani haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Waziri Ummy.
Alitoa rai kwa jamii kuwaheshimu na kuwathamini wanawake kwakuwa ni mama zao, dada zao, shangazi zao na binti zao na suala hilo halivumiliki.
Aliwataka wanaosambaza video hiyo, wasiendelee kufanya hivyo kwani ni udhalilishaji mkubwa wa wanawake na wasichana.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilary, jana aliomba mwongozo kufuatia majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Hamis Kigwangalla, kwamba ni ya uongo bungeni.
Alisema Naibu Waziri huyo alisema vituo vya afya vinne vilivyojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa mkoani Rukwa kwamba majengo yameshindwa kufunguliwa kutokana na taratibu za makabidhiano kutokamilika.
Mbunge huyo alisema anachokijua ni kwamba majengo hayo yamekabidhiwa miaka miwili iliyopita wakati Mkuu wa Mkoa akiwa Mhandisi Stella Manyanya, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Elimu.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, alisema majibu ya mwongozo huo yatatolewa baadaye.

0 comments:
Post a Comment