Taasisi
ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) imebaini kuwepo kwa sukari
iliyofichwa tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Sukari
Kilombero.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam
na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentine Mlolowa Taasisi hiyo imeanza
uchunguzi dhidi ya swala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi
ilitembelea maghala yaliyopo Tabata Jijini Dar es salaam na kubaini
uwepo wa sukari hiyo.
TAKUKURU tayari imetembelea Maghala ya
mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa
wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa kuficha
bidhaa hiyo.
Aidha uchunguzi uliofanywa na Taasisi hiyo ulibaini
kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika maghala
hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala
ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari hiyo ili
iweze kusambazwa.
Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa katika eneo
la Kitumbini kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji bidhaa hiyo na
wachache sana waliweza kuuziwa licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.
Katika
uchunguzi wake TAKUKURU pia imebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati
iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka
viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo
kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi
jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.
Kuficha bidhaa ni
kosa la uhujumu uchumi na ni kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza
Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002]. Serikali
haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua hatua kali dhidi ya
mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii.
TAKUKURU
inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya
kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na
yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa
Sheria.
Home
News
Slider
TAKUKURU yanasa tani za Sukari 4,579.2 zilizofichwa kwenye Maghala ya Tabata na Mbagala.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment