Rais
Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa
miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika
Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la
Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.
Marehemu Lucy
Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya
kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema
katika familia.
Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe
Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango
wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi
ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu
kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment