Tanzania inaadhimisha siku ya uhuru wa Habari jijini Mwanza.
TANZANIA inaungana na Mataifa mengine katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika Jijini Mwanza.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa MOHAMED CHANDE OTHMAN ndiye mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho Siku ya uhuru Vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Maadhimisho ya Mwaka huu kubwa linalohimizwa na wadau wa Habari nchini ni kuitaka Serikali kuharakisha kupitisha Sheria ya Vymbo vya Habari kwa kuzingatia maoni yanayotokana na mapendekezo ya wadau mbalimbali.
Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaenda sambamba na matukio muhimu matatu ya kihistoria ya kuadhimisha miaka 250 ya Sheria ya kwanza ya uhuru wa Habari Duniani, ambapo kauli mbiu inasema “kupata Habari ni haki yako ya msingi.
WAKATI kilele cha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani kikiendelea jijini Mwanza,katibu wa baraza la habari Tanzania MCT-KAJUBI MUKAJANGA amesema kuwa uwepo wa vikwazo mbalimbali katika uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo uingiliwaji wa urushwaji wa matangazo ya bunge moja kwa moja unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa urudishwaji nyuma wa mafanikio yaliopatikana katika tasnia ya habari nchini.
Mukajanga amesema kuwa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa Habari na serikali wana kazi kubwa ya kulinda mafanikio yaliopatikana katika tasnia hiyo kwa faida ya nchi hasa kwa kuhimiza sera bora na utawala wa sheria.
Ameongeza kuwa inapaswa kila idara na taasisi kutambua majukumu yake na kuacha kuingilia baadhi ya kazi na majukumu ya taasisi au chombo flani.
0 comments:
Post a Comment