Leo
Rais wa JAMHURI YA WATU WA CONGO JOSEPH KABILA ametoa nishani Maalum ya
heshima kwa Mwanamziki nguli wa nchi hiyoJules Shungu Wembadio Pene
Kikumba (PAPA WEMBA) aliefariki dunia jumapili iliyopita nchini Ivory
coast wakati akitumbuiza.
Tuzo hiyo ametoa katIka ukumbi wa BUNGE LA
nchi hiyo ulipo kwenye mjii mkuu wa KINSHASA ambako Mwili wa Mwanamziki
huyo uNaagwa kwa heshima maalum ya Serikali na wabunge.
Siku ya
leo jumanne mwili wa PAPA WEMBA unapelekwa kwenye eneo la matongee eneo
ambalo aliishi akiwa mtoto na wananchi watapata nafasi ya kuuga na
kuzikwa siku ya jumatano hapo hapo jijini KINSHASA.
Maelfu ya
waombolezaji wamefurika kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya
mwanamuziki nyota wa muziki wa Soukus na Rhumba raia wa Jamhuri ya Congo
Papa Wemba.
Waomboloezaji walipiga foleni ilikupata fursa ya kutoa
heshima zao za mwisho kwa msanii huyo nguli aliyeaga dunia juma
lililopita alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko Abidjan Ivory
Coast.
Mwili wake umewekwa katika majengo ya bunge mjini Kinshasa.
Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi kuanzia leo hadi jumatano atakapozikwa.
Msanii
huyo nguli alikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa Soukus nchini DRC na
kote duniani kwa kipaji chake cha kipekee na sauti isiyokuwa na mfano.
Wengi waliitambua sauti hiyo ya na utunzi wake.
Alikuwa ni mtumbuizaji kamili.
Gwiji huyo wa muziki wa Lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Yeye alianza kazi ya muziki akiwa na umri mdogo mno.
Alikuwa akimfuata mamake katika matanga na hivyo akaibukia kuwa mtunzi wa nyimbo za kuomboleza.
Mfalme huyo wa muziki wa Rhumba, mwenye umri wa miaka 66 aliaga dunia ghafla 24 April akiwa nchini Ivory Coast.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment