Leicester
City watajizolea $200m (£150m) baada yao kufanikiwa kushinda Ligi Kuu
ya Uingereza Jumatatu, watathmini wa michezo na utangazaji wa Repucom
wanasema.
Pesa hizo zinatokana na tuzo ya kushinda Ligi ya Premia,
pesa za kushiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, na ongezeko la mapato ya
kila siku kutokana na mauzo ya tiketi.
Klabu hiyo pia itajivunia kupanda kwa thamani ya udhamini na pia ongezeko la mashabiki duniani.
Klabu
hiyo inayotoka East Midlands itashiriki katika Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya msimu ujao jambo litakalowawezesha kutazamwa na watu wengi zaidi
kwenye runinga Ulaya na kote duniani.
Afisa mkuu wa ushauri wa
kitaalamu wa Repucom Uingereza na Ireland Spencer Nolan anasema kwamba
mashabiki huwa na umuhimu mkubwa kwa klabu na watachangia sana katika
ukuaji wa Leicester kibiashara.
“Ingawa ni mapema sana kubaini
ongezeko la mashabiki hasa bara Asia, mitandao ya kijamii inatupa fursa
ya kufanya hili,” anasema.
Msimu huu, wafuasi wa Leicester City
katika Facebook waliongezeka 540%, ongezeko kubwa zaidi miongoni mwa
klabu za michezo duniani.
Nchini Algeria klabu hiyo ina wafuasi
500,000 kwenye Facebook, idadi kubwa zaidi katika nchi moja (16.7%),
sana kutokana na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa PFA, winga
Riyad Mahrez ambaye ni raia wa Algeria.
Kumeshuhudiwa pia ongezeko kubwa la mashabiki Thailand na Italia.
Mmiliki wa klabu hiyo Vichai Srivaddhanaprabha ni raia wa Thailand naye meneja Claudio Ranieri ni Mwitaliano.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment